Wanae Col Gaddafi 'hawako Algeria'

Aisha Gadaffi
Image caption Aisha Gadaffi

Wanae Col Muammar Gaddafi watatu na mjane wake wameshaondoka Algeria, balozi wake aliyeko Libya amesema.

Watoto hao ni Hannibal, Mohamed, Aisha na mjane Safia. Aisha na Hannibal wanasakwa na polisi wa kimataifa wa Interpol baada ya serikali ya Libya kuomba wakamatwe.

Balozi Abdel-Hamid Bouzaher alisema kwamba familia hiyo iliondoka "kitambo sana", lakini hakutoa habari zaidi.

Mapema wiki hii, binamuye Col Gaddafi, Ahmed Gaddaf al-Dam, alikamatwa nchini Misri.

Wanne hawa walitorokea Algeria mnamo 2011 baada ya waasi kuvamia mji mkuu wa Libya, Tripoli, mapigano yaliyomaliza utawala wa Gadaffi wa miaja 42. Haijulikani walipo.

Mtoto mwingine wa kiume - Saadi – alitorokea Niger baada ya vita na ndipo alipo hadi sasa.