Utata kuhusu zana za kemikali Syria

Jengo lililoharibiwa Allepo
Image caption Jengo lililoharibiwa Allepo

Maafisa wa serikali ya Marekani wanasema hawaamini kuwa zana za kemikali zilitumika katika shambulio lililotokea nchini Syria Jumanne.

Baada ya kukusanya ushahidi kuhusu kilichotendeka siku hiyo, maafisa hao waliwaambia waandishi wa habari kuwa hawewezi kuthibitisha taarifa hiyo kikamilifu.

Mapema Alhamisi Umoja wa Mataifa ulisema kuwa utaendelea kufanya uchunguzi zaidi iwapo zana za kikemikali kweli zilitumika.

Serikali ya Syria ilisema kuwa waasi walirusha kombora lililokuwa na sumu ya kemikali katika kijiji kimoja kilichoko karibu na Aleppo, na kuwaua watu 26.

Waasi, kwa upande wao, wamekanusha hayo na kulaumu serikali kwa kutumia kemikali aina hiyo hiyo katika mashambulizi yake.