Mashtaka ya wanasiasa wa Kenya yangalipo

Bibi Fatou Bensouda, mkuu wa mashtaka wa Mahakama ya Jinai ya Kimataifa, ICC, ameiambia BBC kwamba kuna mashtaka ya kutosha dhidi ya rais mteule wa Kenya, Uhuru Kenyatta.

Anakabili mashtaka katika ICC kwa uhalifu dhidi ya binaadamu kutokana na uchaguzi wa mwaka wa 2007.

Kesi dhidi ya mshtakiwa mwengine, Francis Muthaura, ilifutwa awali mwezi huu.

Mawakili wa Bwana Kenyatta wanasema mashtaka kama hayo dhidi ya mteja wao yanafaa nayo kutupuliwa mbali.

Hata hivyo, Bi Bensouda alisema kuna ushahidi wa kutosha kumshtaki mwanasiasa huyo na kwamba mashahidi wanafaa kulindwa.

Alisema madaraka mepya hayatabadilisha msimamo wa ICC:

" Kumchagua mshtakiwa wa ICC kuwa rais au makamo wa rais hakutafanya mashtaka kutoweka.

Mashtaka yangalipo kwa sababu tunajaribu kuwapa haki wanyonge katika uhalifu huu.

Bahati mbaya ni kwamba katika majadiliano haya tunawasahau wanyonge."