CAR:Michel Djotodia ajitangaza kuwa rais

Kiongozi wa waasi wa Seleka Michel Djotodia
Image caption Kiongozi wa waasi wa Seleka Michel Djotodia

Waasi walionyakua utawala katika Jamhuri ya Afrika ya Kati mnamo Jumapili wamesema kwamba makubliano yaliyofanywa Januari yaliyounda utawala wa pamoja kati yao na serikali hayatabadilika.

Msemaji Erick Massi aliiambia BBC kwamba kiongozi wa waasi, Michel Djotodia, ambaye ameshajitangaza kuwa rais, anapanga kufanya uchaguzi wa kidemokrasia, lakini hajasema utafanywa lini.

Inaaminika Rais Francois Bozize alitorokea DR Congo.