Nduguye Oscar Pistorius Mahakamani

Image caption Nduguye Oscar Pistorius Carl Pistorius akiwa nje ya nyumba ya Oscar

Nduguye mwanariadha wa Afrika Kusini anayekabiliwa na kesi ya mauaji, Oscar Pistorius, Carlo Pistorius amefikishwa mahakamani kufuatia ajali ya barabarani iliyosababisha kifo cha mwendesha pikipiki mwaka 2008.

Carl Pistorius huenda akafunguliwa kosa la mauaji ya mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 36, katika ajali ya barabarani karibu na Johannesburg.

Wakili wake anasema kuwa Carl hana hatia.

Katika kesi nyingine dhidi ya Oscar Pistorius. mwanaridha huyo amepatikana na kosa la mauaji la ya mpenzi wake mwezi jana , kosa analokanusha vikali.

Mnamo Alhamisi, mawakili wa bingwa huyo wa riadha, wanatarajiwa kupinga vikwazo alivyowekewa kuhusu dhamana yake.

Vyombo vya habari vimetangaza sana taarifa ya kesi inayomkabili Pistorius kwa sababu ya sifa zake kama mwanariadha shupavu.

Wendesha mashtaka wanasema kuwa Carl Pistorius alikuwa anaendesha gari lake katika bustani la Vanderbijl mwezi Machi, mwaka 2008 wakati alipogongana na mwendesha pikipiki Marietjie Barnard, ambaye baadaye alifariki akipokea matibabu hospitalini.

Kesi hii ya Carl ilitupiliwa mbali zamani lakini baada ya viongozi wa mashtaka kupata ushahidi zaidi ndiposa wakafungua upya kesi hiyo.

Familia ya Pistorius ilisema kuwa Carl alisikitika sana kutokana na ajali hiyo lakini ikasisitiza kuwa ilikuwa tu ajali mbaya.