Wanajeshi 11,000 watahitajika Mali

Image caption Wanajeshi hao watapambana na makundi ya wapiganaji wanaotoshia kufanya ugaidi

Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon, amesema kuwa takriban wanajeshi 11,000 huenda wakahitajika nchini Mali kusaidia kuzuia tisho la makundi ya kigaidi.

Walinda amani hao huenda wakahitaji ili kusaidiwa na jeshi lengine ambalo litaweza kufanya juhudi zao katika kukabiliana na harakati za makundi ya kigaidi.

Ufaransa ilituma wanajeshi kwenda Mali mwezi Januari, ili kujaribu kutwaa udhibiti wa maeneo yaliyokaliwa na wapiganaji wa kiisilamu

Inalenga kuanza kuwaondoa wanajeshi hao elfu nne mwezi ujao na kulipatia usukani jesji la muungano wa Afrika.

Ikizingatiwa hali na ukubwa wa tisho la wapiganaji wa kiisilamu, itakuwa muhimu kuwa na kikosi kando na wanajeshi wanaoshika doria kuendesha shughuli sawa na hizo.

Wapiganaji hao sasa wameanza kufanya mashambulizi ya kuvizia kama hatua ya kujibu mashambulizi yanayofanywa dhidi yao na wanajeshi wa Ufaransa.

Mshambuliaji wa kujitoa mhanga alijilipua karibu na kituo cha polisi kushikia doria mjini Timbuktu wiki jana.

Nigeria pia imepeleka wanajeshi wake nchini Mali, lakini hawajahusika na mapigano katika eneo la Kaskazini mwa nchi.

Katika ripoti yake,kwa baraza la usalama la umoja wa mataifa, bwana Ban alipendekeza kuwa wanajeshi wa Afrika nchini Mali wanapaswa kuhudumu chini ya sheria za Umoja wa Mataifa.

Alisema kikosi hicho kinapaswa kuwa na wanajeshi 11,200.

Ban aliongeza kuwa wanajeshi hao watafanya kila wawezalo kuhakikisha kuwa, Umoja wa mataifa unatakeleza jukumu lake la kimataifa.

Duru za kidplomasia zimesema kuwa Ufaransa huenda lkatoa idadi nyingine ya wanajeshi kwa ajili ya kuwepo kikosi kingine kidogo kinachofanya kazi sambamba na kikosi kingine kikubwa cha wanajeshi.

Makundi ya wapiganaji yalitumia pengo lililowachwa wazi wakati wa mapinduzi ya kijeshi na kuanza kudhibiti maeneo ya Kaskazini mwa nchi.