Uchumi wa Cyprus wanusurika

Image caption Mkutano wa rais wa Cyprus na baraza lake la mawaziri

Rais wa Cyprus Nicos Anas ta siades amesema mpango wa kukwamua uchumi ulioafikiwa na wafadhili wa kimataifa umekabiliana na msukosuko wa kiuchumi katika taifa hilo la kisiwani.

Anas ta Siades pia amesema Cyprus haina mpango wowote wa kuondoka katika eneo la Euro.

Lakini amewakashifu wanachama wengine wa eneo la Euro kwa kuagiza mambo mengi kutoka kwa Cyprus.

Wakati mabenki Cyprus yamefunguliwa kwa mara ya kwanza katika muda wa wiki mbili rais Nicos Anas ta siades aliwashukuru wananchi kwa kile alichokitaja kuwa kukomaa kwao.

Kulikuwa na mistari mirefu ya watu waliokuwa wakitaka kutoa fedha katika mabenki hayo