Wachimba migodi 14 wafukiwa na mgodi Arusha

Image caption Wafanya kazi wa migodini hukumbwa na matatizo ya vifaa

Mgodi uliokuwa na wachimba migodi 14 umeporomoka katika eneo la Moshono , mjini Arusha Tanzania.

Hadi kufikia sasa wakati shughuli za uokozi zikiwa bado zinaendelea, maiti watatu wameweza kuondolewa kutoka kwenye mgodi huo.

Mwandishi habari aliyeshuhudia shughuli hiyo ya uokozi, Ali Shemdoe anasema kuwa pia lori mbili zimefukiwa.

Hii sio ajali ya kwanza ya mgodi kutokea Arusha, nyingine ilitokea miaka saba iliyopita na kusababisha vifo vya watu saba.