Idadi ya waliofariki yaongezeka TZ

Image caption Jengo hilo lilikuwa na ghorofa zaidi ya zilizoruhusiwa

Maafisa nchini Tanzania wanasema kuwa takriban maiti thelathini wamepatikana kutoka kwa vifusi vya jengo lililoporomoka mjini Dar es Salaam Ijumaa.

Hata hivyo duru zinasema kuwa maiti 34 wamepatikana. Hadi sasa watu kumi na saba pekee ndio wamepatikana wakiwa hai katima jengo hilo.

Wengine wengi bado hawajapatikana. Wengi wa waliouawa walikuwa wapita njia au wajenzi.

Watoto waliokuwa katika uwanja wa kuchezea uliopakana na jengo hilo, walikuwa miongoni mwa waathiriwa.

Polisi wanasema kuwa wamewakamata watu wanne baada ya rais Jakaya Kikwete kutembelea eneo la janga na kuwataka maafisa wa utawala kuwachukulia hatua waliohusika na ujenzi huo.