Mashujaa na kilio Afrika Kusini

Image caption Wanajeshi wa Afrika Kusini waliouawa katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo

Afrika Kusini ni nchi inayojitegemea pakubwa. Watu hapa hueongea bila kupinda maneno kuhusu kwenda Afrika wakati watakapotafuta maisha tofauti katika bara lisilo na mwelekeo kuelekea Kaskazini.

Hivyo sio kumaanisha kuwa, Afrika Kusini haijihusishi na maswala ya nchi zingine za Afrika, au kutuma majeshi yake kwa opereshini za kulinga mani na ambazo zinagharimu mamilioni ya dola mfano Darfur nchini Sudan.

Lakini inafanya hivyo, angalau machoni mwa umma na hufanya hivyo bila kuzingatia mambo mengi tu.

''Hatujazoea kuona wanajeshi wetu wakiletwa hapa kwa majeneza,'' alisema raia mmoja

Lakini sasa nchi hii imeshangazwa sana na habari za wanajeshi wake 13 kuuawa mwezi jana wakati wa harakati za mapinduzi katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati.

Kiasi cha watu kuanza kuhoji mambo kadhaa, maswali ya hasira kuhusu nini hasa walichokuwa wanafanya wanajeshi hao katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati, na kwa nini hawakuondolewa wakati hali ya usalama ilipozorota.

Madai ya kushangaza yaliyotolewa ni kuwa, walikuwa sehemu ya maslahi ya kibiashara ya chama tawala ANC na rais aliyeng'olewa mamlakani Francois Bozize.

"We are not used to seeing our soldiers coming home in body bags," said Nick Dawes, editor of the Mail and Guardian newspaper that is asking some of the toughest questions of the South African authorities.

"Watu wana wasiwasi mkubwa. Nadhani serikali na chama tawala sasa wanagundua ukubwa wa tatizo walilosababisha amblo ndio sababu ya watu kufanya walivyofanya leo, waliangua kilio ,'' alisema Nick Dawes mhariri wa jarida la Mail

Kilio hicho anasema bwana Dawes, kilijotokeza baada ya nakala jarida la Mail kuchapisha taarifa kuwa ANC inahusika na biashara mjini Bangui. ANC kilifananisha madai hayo kama kukojolea wanajeshi mashujaa wa nchi.

Image caption Waasi wa Jamuhuri ya Afrika ya kati walimng'oa mamlakani rais Fracois Bozize

Rais Zuma alisisitiza kuwa wanajeshi hao ni mashujaa waliofariki kwa kupigania nchi, kuendeleza amani na uthabiti barani Afrika.

Zuma pia alihoji haki ya waandishi wa habari kuchunguza serikali kuhusiana na maswala ya usalama.

"tatizo la Afrika Kusini ni kuwa kila mtu anataka kuongoza nchi, alisema akiteta kuwa ANC ikiwa na wingi wa wabunge bungeni, kinapaswa kuewa nafasi kufanya kazi yake. ''

Baadhi bila shaka wataitikia hili. Lakini wengine watayaona matamshi haya kama ya kibinafsi sana.

Na wengi bila shaka watakubaliana kuwa njia mwafaka ya kuonyesha heshima za mwisho kwa wanajeshi hao ni kuhakikisha kuwa ukweli unajulikana kuhusu kupelekwa kwa wanajeshi wa nchi hiyo katika Jamuhuri ya kidemokrasia ya Congo.

Je bunge la Afrika Kusini, chama cha ANC na upinzani walikosa kupiga darubini?

Je uongozi wa jeshi la Afrika Kusini umekabwa koo kisiasa?

Na je ni kweli mikataba haramu ya kibiashara iliafikiwa katika nchi yenye misukosuko ingawa yenye utajiri mkubwa wa madini ilisababisha moja ya kashfa ambazo huenda zikawa mbaya zaidi kuwahi kutokea katika jeshi la nchi tangu enzi ya ubaguzi wa rangi?