Mgororo wa Korea mbili watokota

Image caption Dereva huyu ni mmoja wa wale waliozuiwa kuvuka kwenda upande wa Korea Kasakazini

Korea ya kusini imesema kuwa nchi jirani ya Korea Kaskazini inawazuia raia wake kwenda kazini upande wa pili wa mpaka katika kiwanda.

Wizara inayohusika na kuleta utangamano kati ya nchi hizo mbili mjini Seoul, imetoa wito kwa serikali ya Pyong Yang itawaruhusu raia hao wa Korea Kusini kurejelea kazi katika kiwanda cha Korean Kusini .

Meneja wengi wa kiwanda hicho wamesusia kwenda kazini wakihofia kuwa watazuiwa kuingia.

Awali Marekani ilitoa onyo kwa Korea Kaskazini dhidi ya kufungua upya kinu cha kutengenezea silaha za nuclear.

Waziri wa nchi za kigeni wa Marekani John Kerry amesema kuwa iwapo Korea Kaskazini itaendelea na mipango yake iliyotangaza hapo jana ya Nuclear, basi utakuwa uchokozi wenye madhara makubwa.

Marekani imeshutumu Korea ya Kaskazini kuhatarisha maisha ya watu bila kujali.

Hapo awali vitisho kutoka kwa Korea Kaskazini, vimekuwa vikipuuzwa tu kama vitisho vya kawaida lakini sasa Marekani imeanza kuwa na wasiwasi kuhusiana na kiongozi chipukizi wa Korea Kaskazini Kim Jong Un , kuwa huenda vitisho vyake sio vya bure.

Akiongea na mwenzake wa Korea Kusini, waziri wa mashauri ya kigeni, wa Marekani , John Kery alitaja kuwa vitosho vya hivi maajuzi ni vya ukweli fulani , na hatari bila kujali lolote.

Alisema kuna muda wa kutosha kwa Korea Kasakazini kubadili mwenendo wake ili kutilia mkazo zaidi mahitaji ya watu wa eneo hlo ambayo Kerry alisema Marekani iko tayari kusaidia.

Lakini ushawishi wa kurejesha misaada huenda usibadilishe msimamo wa Korea Kaskazini. Marekani imetaka Uchina ishauriane na jirani wake wa Korea Kaskazini . Kwa wakati huu Marekani inaendelea kunyosha misuli yake ya kijeshi .

Makao makuu ya Jeshi la Marekani , Pentagon yalithibitisha yatatuma zana nyingine za kuharibu makombora katika eneo hilo.