Vifo kutokana na Saratani vinaweza kuzuiwa

Watafiti kutoka Marekani na Sweden wanasema karibu nusu ya vifo vinavyotokana na saratani ya kibofu vinaweza kuepukika kwa kufanya uchunguzi kwa wanaume walio na umri wa miaka zaidi ya arobaini .

Hata hivyo Swala hilo bado lina utata kwa sababu njia ya uchunguzi huo ambayo ni kupima kiwango cha protini kwenye damu , si ya kuaminika .

Lakini watafiti wanasema kuwa ni vyema kwa wanaume wenye miaka zaidi ya arobaini kufanyiwa uchunguzi huo.

Wanasema kuchelewa kwa uchunguzi hadi wanaume wafikie miaka 50 kunapunguza uwezekano wa kubaini saratani hiyo katika kiwango cha kuweza kutibiwa , huku kuwafanyia uchunguzi wanaume vijana huenda kusitoe matokeo sahihi.

Taariifa hii inafuatia uchunguzi uliofanywa kwa wanaume wa Sweden zaidi ya elfu 21 kwa muda wa miaka thelathini