Familia iliyotekwa nyara yaachiliwa Cameroon

Image caption Ramani ya Cameroon

Familia moja ya watu saba kutoka Ufaransa waliokuwa wametekwa nyara nchini Cameroon imeachiliwa kwa mujibu wa maafisa kutoka nchi hizo mbili.

Waziri wa mawasiliano nchini Cameroon, Issa Tchiroma Bakary aliambia BBC kuwa walikuwa katika hali nzuri bila ya majeraha yoyote.

Familia hiyo ikiwemo watoto wanne , walitekwa nyara mwezi Februari, na watu waliokuwa wamejihami kwenye pikipiki baada ya ziara yao katika mbuga ya wanyama Kaskazini mwa nchi hiyo.

Katika video iliyowekwa kwenye mtandao wa YouTube, wanamgambo kutoka Nigeria Boko Haram walidai kuwateka watu hao.

Taarifa ya kuachiliwa kwa mateka hao, pia ilitangazwa kupitia redio ya taifa ya Cameroon siku ya Ijumaa.

Taarifa kutoka kwa rais, familia hiyo ilikabidhiwa kwa maafisa wakuu wa serikali siku ya Alhamisi.

Kulingana shirika la habari la Associated Press, serikali za Nigeria na Ufaransa zilipewa shukrani katika taarifa hiyo.

Familia hiyo inaishi mjini Yaounde ambako babao alifanya kazi na kampuni ya gesi ya Suez, na huko ndiko walitekwa nyara tarehe 19 mwezi Februari.

Wanajeshi wa Cameroon walizingira gari walimotekwa nyara