Israel yaishambulia tena Syria

Syria imeishutumu Israel kuwa inawasaidia wapiganaji kijeshi, baada ya Israel kushambulia maeneo kando ya Damascus.

Wizara ya mashauri ya nchi za nje ya Syria ilisema mashambulio ya Israel yalilenga vituo vitatu vya jeshi kando ya mji mkuu, na kuuwa na kujeruhi watu.

Wizara hiyo ilisema uhasama wa Israel unaonesha kuwa nchi hiyo inashirikiana na magaidi na Waislamu wenye msimamo mkali.

Hili ni shambulio la pili kufanywa nchini Syria katika siku chache.

Israel haikusema kitu.

Katibu Mkuu wa Jumuiya ya nchi za Kiarabu, Nabil al-Arabi, amelaani kile alichoita uhasama wa wazi wa Israel.