Kenya yawafunga maisha raia wa Iran

Image caption wa Iran

Raia wawili wa Iran wamehukumiwa kifungo cha maisha katika mahakama moja ya Kenya kuhusiana na mashtaka ya ugaidi.

Raia hao ni Ahmad Mohammed na Sayed Mousavi ambao walishtakiwa wiki iliyopita kwa kumiliki vilipuzi, ambavyo inaaminika vilikuwa vitumiwe kwa kufanya mashambulizi.

"mwili unanisisimka nikifikiria hasara ambayo ingesababishwa na shambulizi hilo la kigaidi," amesema jaji Kiarie Waweru Kiarie, kama linavyoripoti shirika la habari la AFP.

Hata hivyo, serikali ya Iran imekana kuhusika na mpango huyo wa kuishambulia nchi ya Kenya.