Uchumi wa Ufaransa taabani

Image caption Ufaransa inakabiliwa na changamoto za kiuchumi

Nchi ya Ufaransa ambayo ni ya pili kwa ukubwa wa uchumi wake katika kanda ya Euro, imethibitisha kuwa uchumi wake unadorora.

Uchumi wa Ufaransa haujakuwa kwa kiwango kizuri kwa zaidi ya mwaka mmoja, na mwisho ilishuhudia mdororo mwanzoni mwa mwaka 2012.

Habari hizi zinakuja wakati nchi hiyo ikiadhimisha mwaka mmoja wa utawala wa rais Francois Hollande.

Duru zinasema kuwa sababu za uchumi wa Ufaransa kudorora zinatokana na wanunuzi kukosa imani pamoja na ongezeko la viwango vya ukosefu wa ajira na kufikia asilimia 11.

Kanda ya Euro, kwa ujumla wake inaendelea kuathirika na kuduma kwa uchumi wake huku takwimu kutoka kwa nchi yenye uchumi mkubwa katika kanda hiyo Ujerumani, ikionyesha ukuwaji wake ukijikokota kwa asilimia sufuri nukta moja mwanzoni mwa mwaka.