Mapigano kati ya wapiganaji wa Mali

Mapigano yamezuka kaskazini mwa Mali baina ya kundi kuu la wapiganaji wa kabila la Tuareg, MNLA, na wapiganaji Waarabu wa kanda hiyo.

Msemaji wa MNLA, Moussa Ag Assarid, alieleza kuwa wapiganaji wao walishambuliwa katika mji wa Anefis na wapiganaji wa Kiislamu hapo jana na kwamba mapambano yanaendelea.

Waandishi wa habari wanasema ghasia hizo zinaonesha vipi wapiganaji waliokimbia mashambulio yaliyoongozwa na kikosi cha Ufaransa dhidi ya wapiganaji wa Kiislamu na Watuareg, bado wanachafua juhudi za kurejesha amani nchini Mali kabla ya uchaguzi wa mwezi July.