Wanne wafa kwenye msongamano kanisani

Watu wane wamekufa na 13 kujeruhiwa katika mkanyagano ndani ya kanisa la kiavengalisti nchini Ghana.

Ajali hiyo ilitokea pale waumini walipoania kufikia maji matakatifu katika tawi la kanisa la Synagogue Church of All Nations (SCOAN) katika mji mkuu, Accra.

Ripoti zinasema maelfu ya watu walikuwa wamekwenda kanisani humo.

Kanisa hilo liloanzishwa na kasisi wa Nigeria, TB Joshua, ambaye anasema yeye ni mtume.

Piya amezusha utata kwa kudai kuwa anaweza kutibu magonjwa yasiyotibika kama HIV na UKIMWI.