Polisi wa Nairobi wauwa washukiwa wawili

Polisi wa Nairobi wakiwa kazini

Polisi mjini Nairobi, Kenya, wamewapiga risasi na kuwauwa watu wawili - mwanamume na mwanamke - baada ya watu hao kurusha maguruneti mane na kuwajeruhi askari kama watano.

Polisi walivamia fleti wanakoishi watu hao kwenye kitongoje cha mji na waliwaamrisha watoke nje ya fleti.

Wakuu wa polisi wanasema wawili hao walikataa kusallim amri, walirusha maguruneti na walimtumia mtoto wao mchanga wa miezi minane kuwa kinga.

Haijulikani kama watu hao wawili wanahusika na kundi lolote la wapiganaji.

Magazeti ya Kenya yanaarifu kuwa kisa hicho kilitokea katika Githurai estate.