Huwezi kusikiliza tena

Maandamano ya kupinga unyanyapaa Kenya

Umoja wa Ulaya umetaka hatua zichukuliwe kupambana na unyanyapaa wa wapenzi wa jinsia moja.

Hii ni kutokana na utafiti uliofanywa na kuonesha unyanyasaji mkubwa unaofanywa dhidi ya wapenzi wa jinsia moja.

Hali hiyo inakuja siku moja baada ya maandamano ya wapenzi wa jinsia moja kufutwa nchini Georgia kabla hata hayajaanza.

Maandamano hayo yalizongwa na waandamanaji wanaopinga mapenzi ya jinsia moja. Nchini Kenya yamefanyika maandamano pia kama hayo ya kupambana na unyanyapaa. Maandamano hayo pia hayakufika mbali, kama anavyoeleza Anne Mawathe.