Kagame akosoa kikosi cha UN DRC

Image caption Rwanda imekuwa ikikana mara kwa mara tuhuma kuwa inahusika na vita DRC

Rais wa Rwanda Paul Kagame alitoa mtazamo mkali wa ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa mataifa ulioko katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Kagame ameiambia BBC kwamba kikosi cha Umoja wa Mataifa cha askari elfu 20 kilichopelekwa miaka 14 iliyopita, hakijafanya lolote kutatua chanzo cha matatizo ya Congo na wakati mwingine kimeufanya mzozo huo kuwa mmbaya zaidi.

Amesema visa vya mapigano , ghasia, na watu kupoteza makaazi yao kulitishia usalama wa eneo zima.

Serikali ya rais Kagame imekana mara kwa mara tuhuma za Umoja wa mataifa na makundi ya kutetea haki za binadamu kwamba Rwanda inawasaidia wanamgambo mashariki mwa Congo.

Rais Kagame amesema kuwa kutumia nguvu kungesaidia ikiwa tu inekuwa inalenga kusaidia msimamo fulani wa kisiasa.