Viongozi wa AU waanza mazungumzo

Baada ya sherehe za Jumamosi mjini Addis Ababa kuadhimisha miaka 50 tangu kuanzishwa kwa Umoja wa Afrika, viongozi wa Afrika sasa wanajadili baadhi ya matatizo yanayokabili bara hilo.

Vita vya muda mrefu katika Jamhuri ya Demokrasi ya Congo vilichukua nafasi kubwa mazungumzo yalipoanza.

Tena majadiliano yakahusu pendekezo la kuyafanya mahakama ya jinai ya kimataifa, ICC, yaache hatua za kumfikisha mahakamani rais mpya wa Kenya na makamo wake kwa mashtaka ya uhalifu dhidi ya binaadamu.

Wanabalozi wanasema viongozi wa Afrika wamegawika kuhusu swala hilo.

Mawaziri wa Mashauri ya Nchi za Nje walikubaliana Alkhamisi, kabla ya viongozi kukutana, kwamba AU iiombe ICC kupeleka jukumu la kesi za Rais Uhuru Kenyatta na makamo wake Wiliam Ruto kwa mahakama ya Kenya.