Anzhi Makhachkala inataka Eto'o apumzike

Image caption Samuel Eto'o

Klabu ya Anzhi Makhachkala inayoshiriki ligi kuu ya ya premier nchini Urussi imeiandikia shirikisho la mchezo wa soka nchini Cameroon, kutomshirikisha, nyota wake Samuel Eto'o, katika michuano ya kufuzu kwa kombe la dunia ya mwaka wa 2014.

Kwa mujibu wa daktari wa klabu hiyo, Stijn Vandenbroucke, mshambuliaji huyo alipata jeraha mbaya la mguu wakati wa mechi yao ya fainali ya kuwania kombe la Shirikisho nchini humo siku ya Jumamosi.

Daktari huyo amependekeza kuwa mchezaji huyo apewe wiki kadhaa za kumpumzika.

Eto'o anatarajiwa kusafiri nchini Cameroon, siku ya Jumatatu ili kufanyiwa uchunguzi wa kimatibabu na madaktari wa timu ya taifa ya Cameroon, Indomitable Lions.

Madaktari wa timu hiyo ya taifa ndio watakaokuwa na usemi wa mwisho ikiwa Eto'o anaweza kushirikishwa katika kikosi cha Cameroon kitakachochuana na Togo tarehe 9 mwezi huu na dhidi ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo wiki moja baadaye.

Kwa sasa Cameroon, inaongoza kundi I na alama sita alama moja tu mbele ya Libya huku Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo ikiwa na alama nne na Togo ikishika mkia katika kundi hilo na alama moja.

Klabu hiyo ya Anzhi, imesema iko tayari kugharamia matibabu ya Eto'o, Ulaya ikiwa shirikisho la soka nchini Cameroon litaafiki mapendekezo yao.

Eto'o alicheza dakika mia moja ishiriki wakati timu yake iliposhindwa kupitia mikwaju ya penalti katika fainali ya kuwania kombe la Shirikisho dhidi ya CSKA Moscow.