Mourinho ateuliwa kocha mpya wa Chelsea

Image caption Jose Mourinho

Klabu ya Chelsea imethibitisha kuwa Jose Mourinho ametueliwa rasmi kuwa kocha mpya wa klabu hiyo.

Mourinho amesaini mkataba wa miaka minne na anarejea tena Chelsea ambako aliisaidia kushinda kombe la ligi kuu ya premier mara mbili, kombe la FA na mawili ya kombe la ligi kati ya mwaka wa 2007 na 2007.

Afisa mkuu mtendaji wa klabu ya Chelsea, Ron Gournlay, amesema '' Bodi ya wakurugenzi ya Chelsea ina fahari kutangaza rasmi kuwa Jose Mourinho ametuliwa kuwa kocha mpya na ni fahari yai kumkaribisha tena katika klabu hiyo''.

Gournlay aliendelea kusema kuwa, mafanikio yake na nia yake ya kuandikisha matokeo mema zaidi yalimfanya kuwa mgombea anayestahili kupewa nafasai hiyo.

'' Ni nia yetu kusonga mbele na kuifanya klabu yetu ipate matokeo mema zaidi na chini ya uongozi wa Mourinho, naamini kuwa Chelsea itapata mafanikio zaidi kwa kuwa yeye ndiye chaguo letu nambari moja'' Alisema afisa huyo.

Mourinho alikuwa na ufuasi na ushawishi mkubwa wakati na hata baada ya kukihama klabu ya Chelsea.

Wasifu wa Mourinho

Image caption Mourinho akiwa na Real Madrid

Tangu alipokihama klabu ya Chelsea mwaka wa 2007, Mourinho alifanya kazi nchini Italia na klabu ya Inter Milan, kabla ya kujiunga na klabu ya Real Madrid ya Uhispania ambako alishinda vikombe vitatu vya ligi kuu, mawili ya ligi shirikisho na kombe la klabu bingwa barani Ulaya.

Mourinho aliteuliwa kuwa kocha wa Chelsea mara ya kwanza mwaka wa 2004, miezi michache baada ya kushinda kombe la klabu bingwa barani ulaya na klabu ya FC Porto, na February mwaka wa 2005 alishinda kombe lake la kwanza wakati Chelsea ilipoishinda Liverpool kwa magoli matatu kwa mawili katika fainali ya kombe la Carling.

Mwaka huo Chelsea ilishinda ligi kuu ya Premier kwa kuzoa jumla ya alama tisini na tano na kufungwa magoli 15 tu katika mechi Thelathini na nane.

Msimu wa mwaka wa 2005-2006 Chelsea ilishinda tena kombe la ligi kuu kwa taadhima kuu pale ilipoinyuka Machester United magoli matatu kwa bila.

Baada ya hapo Chelsea iliishinda Arsenal katika fainali ya kombe la Carling mjini Cardiff na pia kombe la FA wakati Manchester United haikuwa imepoteza mechi yoyote katika uwanja mpya wa Wembley.

Mwaka wa 2007, Mourinho alijiuzulu baada ya kushauriana na wasimamizi wa Chelsea na kujiunga na klabu ya Inter Milan ya Italia.

Image caption Mourinho akiwa na Frank Lampard

Akiwa na Inter Milan alishinda mataji mawili ya ligi ya Seria A na kombe la klabu bingwa Marani Ulaya.

Kocha huyo kisha alijiunga na Real Madrid ambako alishinda kombe la La Liga na lile la Copa Del Rey na kumaliza majukumu yake kama kocha nchini Uhispania hiyo jana.

Mourinho anarejea Chelsea na baadhi ya maafisa wake wa kiufundi Rui Faria, Silvio Louro na Jose Morais.

Kila mmoja wao atakuwa na jukumu na cheo cha naibu kocha mkuu na watashirikiana na maafisa wanaohudumu na Chelsea kwa sasa ikiwa ni pamoja na Steve Holand, Christophe Lollichon na Chris Jones.

Mourinho atajulishwa rasmi kwa wachezaji na mashabiki wa klabu hiyo tarehe kumi mwezi huu katika uwanja wa Stamford Bridge.