Mjumbe mpya wa UN awasili Somalia

Image caption Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa alizuru Mogadish kwa mara ya kwanza tangu Al Shabaab kufurushwa

Mkuu wa ujumbe mpya wa Somalia katika umoja wa mataifa nchini, amewasili katika mji mkuu Mogadishu kuanza kazi yake.

Nicholas Kay anachukua zamu kutoka kwa Augustine Mahiga aliyekuwa mjumbe maalum wa Umoja wa Matifa nchini Somalia.

Duru zinasema kuwa ujumbe mpya wa Umoja wa mataifa nchini Somalia, (UNSOM) utanuia kuisaidia serikali ya Somalia kuweza kuikarabati nchi hiyo.

Umoja wa mataifa unasema kuwa mashirika yake yote yanayojihusiaha na maswala ya Somalia yatalaziomika kuhamia mjini Mogadishu kutoka Nairobi.

Mji wa Mogadishu umekuwa mtuylivu kwa muda tangu kuondoka kwa wapiganaji wa kiisilamu Al Shabaab kufuatia juhudi za majeshi ya Kenya na yale ya Muungano wa Afrika.

Hata hivyo inaarifiwa licha ya hali kusemekana kuwa bora kuliko miaka ya nyuma, bado kuna tisho la utovu wa usalama kwani Al Shabaab wameanza kutumia mbinu ya mashambulizi ya kuvizia kushambulia mji wa Mogadishu.