Mandela arejeshwa tena Hospitalini.

Image caption Mzee Mandela alipotembelewa na rais Zuma mwaka huu

Rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela amerejeshwa hospitalini mara baada ya kusumbuliwa na ugonjwa wa mapafu kwenye mfumo wake wa kupumua.

Mandela mwenye umri wa miaka 92 aametajwa kuumwa sana lakini akiwa mwenye hali nzuri na amelazwa kwenye hospitali moja ambayo hakutajwa jina huko mjini Pretoria mapema usiku wa kuamkia leo.

Aidha msemaji wa rais huyo wa kwanza mweusi kwenye taifa la Afrika Kusini amesema hali yake ni njema na anaweza kupumua bila kutumia msaada wa mashine maalumu.

Hi mara ya tatu kwa mwaka huu bwana Mandela kulazwa hospitalini ambapo aliwahi kugundulika kuwa na ugonjwa wa kifua kikuu wakati akitumikia kifungo chake cha miaka 27 jela.

Mkewe Bi Graca Machel amehairisha ziara yake mjini London ambako alikuwa ahudhurie mkutano maalumu na inaaminika amerejea Afrika kusini kukaa na mumewe.