Mapigano Kismayo,kumi wafariki dunia.

Image caption Walinda amani mjini Kismayo

Zaidi ya watu kumi wanaripotiwa kuuwawa katika siku ya pili ya mapigano kusini mwa mji wa Kismayo nchini Somalia.

Wakazi wa mji huo wameiambia BBC kuwa mapigano yamezidi kupamba moto. Mamia ya watu wa mji huo wameyakimbia makazi yao.

Vikosi vya kulinda amani vya umoja wa mataifa vimekuwa vikijitahidi kutuliza hali hiyo na utaka maelewano baina ya wapiganaji wa makundi mawili yaliyojitangazia uraisi wa eneo hilo lijulikanalo kama Jubaland.

Rais wa Somalia Hassan Shekh Mahmud amesema mapigano katika eneo la Kismayo yanaathiri juhudi za maendeleo ya nchi zinazofanywa hivi sasa.