Wavuti wa ANC washambuliiwa

Wafuasi wa chama cha ANC
Image caption Wafuasi wa chama cha ANC

Wapinzani wa rais Robert Mugabe wamelenga tovuti ya chama tawala cha Afrika kusini ANC wanacholaumu kuunga mkono rais huyo.

Mtu ambaye hakutaka jina lake litajwe amesema kwamba udakuzi pia imefanywa kwenye tovuti ya wizara ya ulinzi ya Zimbabwe na kwenye gazeti la serikali Herald.

Chama cha ANC imesema wavuti wake umevurugwa na ujumbe unaosambazwa na kampuni ya DDC.