Renamo chahusishwa na mashambulizi Msumbiji

Watu wawili wameuawa katika mashambulizi yanayoshukiwa kufanywa na wapiganaji wa chama cha upinzani cha Renamo, katika mkoa wa kati nchini Msumbiji

Maafisa wakuu wamesema kuwa ufyatulianaji risasi ulitokea siku mbili baada ya mkuu wa habari katika chama hicho, Jeronimo Malagueta kusema kuwa chama hicho kitakwamisha shughuli za usafiri wa barabara na reli kuelekea kwa machimbo ya mkaa.

Polisi walimzuia mapema leo , muda mfupi baada ya mashambulizi kufanyika.

Kundi hilo la zamani lilisitisha vita vya miaka 16 vya wenyewe kwa wenyewe mnamo mwaka 1992.

Lakini hofu ni kuwa mkataba wa amani na chama tawala, huenda ukavunjika na hili lilijitokeza zaidi mwaka jana wakati kiongozi wa Renamo Alfonso Dhlakama, aliporejea msituni.

Siku ya Jumatatu wanajeshi sita waliuawa wakati washambulizji walipovamia karakana ya silaha katika mkoa wa kati wa Dondo; huku ididi kubwa ya silaha zikiibiwa.

Chama cha kilikanusha madai kuwa kilihusika na mashambulizi hayo.

Aidha chama hicho, hakijazungumzia mashambulizi hayo lakini msemaji wake Fernando Mazanga alithibitisha kwa BBC kuwa Bwana Malagueta amezuiliwa.

Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani Pedro Cossa, alisema kuwa watu waliokuwa wamejihami walishambulia magari katika mashambulizi mawaili katika mkoa wa Sofala Kusini mwa Msumbiji.