Raia 2 wa Nigeria wakamatwa nchini Kenya

Image caption Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta

Polisi nchini Kenya wanawazuilia raia wawili wa Nigeria waliopatikana na dawa za kulevya zenye thamani ya shilingi milioni 10 au dola zaidi ya laki moja.

Wawili hao waliokuwa wanaelekea nchini Nigeria kutoka Brazil, walikuwa wamemeza vidonge 54 vyenye Cocain lakini baada ya kuwekwa chini ya uchunguzi wa polisi wakaweza kuvitoa vidonge hivyo.

Wawili hao walikamatwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jomo Kenyatta mjini Nairobi wakitoa Brazil kuelekea mjini Lagos, Nigeria.

Asubuhi ya leo walipelekwa katika mahakama moja mjini Nairobi na kushtakiwa kwa kosa la kumiliki madawa ya kulevya ambayo ni haramu nchini Kenya.

Ni wiki hii tu ambapo mzozo wa kidiplomasia umekuwa ukitokota kati ya Nigeria na Kenya baada ya kufurushwa kutoka nchini humo kwa mfanyabiashara mwenye utata raia wa Nigeria Anthony Chinedu baada ya kuhusishwa na biashara haramu ya madawa ya kulevya.

Chinedu alirejeshwa Nigeria kufuatia amri ya rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta kuwa raia wa kigeni wanaohusika na biashara haramu za madawa ya kulevya wurejeshwe kwao.

Hata hivyo mzozo ulianza pale ndege ya Kenya iliyokuwa imewabeba maafisa wa Kenya waliokuwa wanamrejesha Chinedu nchini Nigeria ilipozuiliwa katika uwanja wa Ngege wa Murtallah baada ya kumfikisha Chinedu nyumbani.

Kwa sasa juhudi za kidiploamsia zinagli zinaendelea kuweza kuwarejesha Kenya maafisa hao. Maafisa wa Nigeria wamezungumzia mzozo huo wakikanusha madai kuwa maafisa wa Kenya waliteswa