Watu 6 wauawa Kaskazini mwa Kenya

Image caption Ramani ya Kenya

Watu sita wameuawa kufuatia mapigano mapya ya kiukoo katika kuanti za Mandera na Wajir Kaskazini mwa Kenya.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Kenya, watu wanne waliuawa, wakati wapiganaji kutoka kwa jamii ya Degodia waliposhambulia lori moja ya mizigo.

Gavana wa Jimbo wa Mandera Ali Roba, watu hao waliuawa hiyo jana na emeongeza kusema kuwa wamepokea ripoti kuwa watu hao waliuawa kinyama.

Mandera County governor Ali Roba said the people were killed during the broad daylight attack on Friday.

Roba amesema watu waliokuwa wakisafiri kwa lori hilo waliviziwa katika eneo la Eldas ambapo wanne waliuawa papo hapo na wengine wanne walifanikiwa kutoroka.

Baada ya kuwauawa watu wao, wavamizi hao waliteketeza lori hilo baada ya kupora mali yote.

Shirika la Msalaba Mwekundi nchini Kenya, waliojeruhiwa wanaendelea kutibiwa katika hospitali ya wilaya ya Mandera.

Katika tukio lingine watu wengine wawili wameuawa katika Kaunti ya Wajir.

Gavana wa eneo hilo amethibitisha tukio hilo na kutoa wito kwa raia wa eneo hilo kudumisha amani.

Mashambulio katika eneo la Kaskazini mwa Kenya yamekuwa yakiongezeka katika miezi ya hivi karibuni, tangu serikali ya Kenya ilipoamua kutuma wanajeshi wake nchini Somalia kupambana na wapiganaji wa Al Shabaab.

Tarehe kumi na moja mwezi huu, watu sita waliuwa kufuatia mapigano hayo ya kiukoo katika jimbo la Mandera.