Maandamano dhidi ya rais Morsi yaanza

Image caption Waandamanaji nchini Misri

Raia wa Misri wamefanya maandamano makubwa kote nchini kumshinikiza rais wa taifa hilo Mohammed Morsi, kujiuzulu wakati wa maadhimisho yake ya kwanza tangu achukue hatamu ya taifa hilo.

Ijapokuwa barabara za mji wa Cairo zina utulivu kufikia sasa, maafisa wa polisi wamewekwa katika kila sehemu ili kuzuia ghasia.

Wapinzani wa rais huyo wanamkashifu kwa kushindwa kutatua maswala ya kimsingi kama vile uchumi pamoja na usalama na kudai kuwa zaidi ya raia millioni 22 wametia sahihi ya kutaka uchaguzi mpya kufanyika mara moja.

Aidha wanadai kuwa rais Morsi, ameweka ajenda ya Kiislamu ya chama chake cha Muslim brotherhood mbele kushinda mahitaji ya raia wa taifa hilo.

Wafuasi wa rais huyo pia wameapa kufanya mikutano ya hadhara kumuunga mkono kiongozi wao.