Habre afunguliwa mashtaka Senegal

Image caption Hissene Habre

Mahakama maalumu nchini Senegal imemfungulia mashtaka ya uhalifu wa kivita,uhalifu dhidi ya binadamu na mateso aliyekuwa rais wa Chad, Hissene Habre.

Jaji wa mahakama hiyo aliamuru awekwe kizuizini kabla ya kuanza kusikilizwa kwa kesi dhidi yake.

Makundi ya kutetea haki yanakadiria kuwa takriban watu alfu arobaini waliuwawa wakati wa utawala wa ki-imla wa bwana Habre uliodumu miaka minane hadi mwaka 1990.

Bwana Habre, ambaye ameishi nchini Senegal kwa kipindi cha miaka 20 alikamatwa siku ya jumapili.