Cameroon yafungiwa na FIFA

Timu ya taifa ya Cameroon
Image caption Timu ya taifa ya Cameroon

Cameroon imefungiwa kwa muda na FIFA kufuatia serikali ya nchi hiyo kujiingiza katika maswala ya chama cha soka nchini humo.

Tangazo la FIFA limesema kwamba kamati ya dharura ya shirikisho hilo la dimba duniani imeamua kusimamisha kwa muda chama cha soka cha Cameroon FECAFOOT na uamuzi huo umeanza kutekelezwa mara moja kwa sababu serikali inaingilia maswala ya chama cha soka.