Mgawanyiko wa kimawazo kuhusu Misri

Watu katika kanda ya Afrika Kaskazini wamegawanyika kuhusu tafsiri ya matukio nchini Misri na mgogoro unaokumba taifa kubwa zaidi la kiarabu , Misri.

Ndani ya Libya , kwa zaidi ya mwaka mmoja unusu uliopita, vijana wamekuwa wakionekana wakigeuka na kuwa wakali kwa chama cha Muslim Brokherhood kinyume na mambo yalivyokuwa hapo nyuma.

Raia wa Libya ambao hawakuchagua wanasiasa wenye misimamo ya kiisilamu, nao pia wameanza kuwashuku sana hawa watu wa Muslim Brotherhood.

Walionekana kuunga mkono hatua ya jeshi kumpindua aliyekuwa rais Mohammed Morsi wa chama cha Muslim Botherhood.

Wananchi wa Libya wamekuwa wakisikika wakisema eti wanataka mapinduzi ya pili , katika mwaka mmopja uliopita.

Lakini wakati wakitoa matamshi kama haya, unashindwa kuelewa ni nani watakayempigia kura, hawana mtu wanayemuona kama anayewaunganisha watu na wala hawana jeshi la kusema nalo.

Wanaoenakana kuwa wanyonge na kutofurahia ambavyo serikali inaendesha mambo, baraza la kitaifa la Congress ambalo walilipigia kura mwaka mmoja uliopita pia halijawafurahisha wakiwemo viongozi wa kijeshi. Na la kukera zaidi ni idadi ya wapiganaji wanaoendelea kuongezeka kila kuchao.

Mgawanyiko wa kimawazo

Kufuatia hatua ya kumwondoa mamlakani rais Mohammed Morsi, rais mmoja wa Libya kwa jina Ibrahim na ambaye pia ni mwanaharakati, aliyesimama mahakamani mjini Benghazi na kuipinga serikali ya Gaddafi mwaka 2011, anasema kwa kauli moja kuwa '' kilichotokea Misri pia kitashuhudiwa Libya.''

Libya bila Gaddafi imeshuhudia maandamano ya kupinga ghasia ingawa ya kuunga mkono serikali.

Na wala haoni hatua ya jeshi nchini Misri kama mapinduzi ya kijeshi.

Image caption Vurugu mjini Cairo

"walichukua hatua, hiyo ili kulinda maslahi ya raia ,'' aliambia BBC.

Hanna Ghallal, wakili kutoka kitovu cha mapinduzi nchini Libya ana msimamo tofauti kuhusu harakati za Misri.

Kama mwanaharakati, anahisi wamisri walimpinga Morsi kwa sababu za kimaadili na demokrasia, kwa sababu hilo halikomi katika sanduku ya kura.

Lakini kama mwanamke huyo wakili, haoni kama hatua ya jeshi ilikuwa sawa , kwa sababu sasa wao ni sehemu ya mzozo na kwamba jeshi halipaswi kupendelea upnade wowote.

Ibrahim na Hanna wanakubaliana kwa kitu kimoja kuwa kuna mgawanyiko wa kimawazo,kuhusu Misri ikikabiliwa na tisho la kutumbukia kwenye mgogoro wa wenyewe kwa wenyewe ambao unaweza kusambaa hadi kwenye mipaka yake.

"ikiwa Misri itasambaratika, hebu tarafakri nini kitafanyika Libya,'' anasema Bi Ghallal. "tunawategemea kwa sababu ya mpaka wetu kwa swala la usalama kwa sababu hatuna jeshi la kukabiliana na utovu wa usalama.''

Dalili za vita vya wenyewe kwa wenyewe

Upande wa Magharibi mwa Misri ni Tunisia ambao tayari wamepiga hatua, ambapo wanaonekana kuiga mfano wa Misri na kuanza harakati za upinzani au Tamarod mfano wa zilizoanzishwa na wanaharakati wa Misri waliofanikiwa kuwashawishi mamilioni ya watu waliomiminika barabarani kutaka mageuzi baada ya miezi kadha ya kampeini.

Taieb Moalla, Mwandishi wa habari wa Tunisia na ambaye kwa muda mrefu amekuwa mpinzani wa rais aliyeng'olewa mamlakani, anashangazwa sana na matukio.

Image caption Kiongozi wa upinzani Misri Mohammed El Baradei

Kama wanavyojua watunisia, mapinduzi hufuatwa na kipindi cha vurugu na suitofahamu kuhusu kinachopaswa kufanywa baadaye.

Ingawa bwana Moalla haoni kama mapinduzi hatua ya kumwondoa mamlakani bwana Morsi, kwa sababu mamilioni waliunga mkono hatua ya jeshi, haamini kwamba jeshi liliingilia mzozo huo kwa sababu za kidemokrasia au eti kulinda watu.

''Kuna dalili za vita vya wenyewe kwa wenyewe,'' alisema . Kuna uwezekano huo kwa sababu kuondolewa mamlakni kwa Morsi kutamfanya kuwa na ushawishi mkubwa miongoni mwa wafuasi wake wa Muslim Brotherhood na kusababisha misimamo mikali.

Mapinduzi huhusishwa na mabadiliko , lakini kwa uhakika hufuatiwa na kipindi cha mgogoro mkali, kuhusu hatua zinazopaswa kuchukuliwa, nani aongoze harakati hizo na namna ya kuziendesha.