'Dunia imeitelekeza CAR,' lasema MSF

Image caption Mji mkuu wa CAR Bangui

Shirika la misaada la Medecins Sans Frontieres, limetoa tahadhari kuhusu hali mbaya ya kibinadamu katika Jamuhuri ya Afrika ya Kati miezi mitatu baada ya chama cha muungano wa waasi kutwa mamlaka.

MSF linasema kuwa hospitali ziliporwa, huku wafanyakazi wa mashirika ya misaada wakikimbilia usalama wao wakati waasi walipokuwa wanatekeleza uasi wao.

Wengi wa watu waliachwa bila huduma za afya.

Utovu wa usalama unaoendelea, unatatiza shughuli ya utoaji chanjo pamoja na mpango wa matibabu huku viwango vya ugonjwa wa Malaria vikipanda.

Licha ya hali kuwa mbaya , MSF linasema kuwa idadi ya mashirika ya misaada katika Jamuhuri ya Afrika ya kati imekuwa ndogo sana ikilinganishwa na siku za nyuma.

Linaitaka jamii ya kimataifa, kujitolea kuimarisha usalama na kupata msaada kwa wale wanaouhitaji zaidi.