Tyson Gay na Asafa Powel walitumia madawa haramu

Image caption Asafa na Gay ni miongoni mwa wanriadha shupavu duniani

Wanariadha wawili kati ya wanariadha wenye kasi kubwa duniani -- Tyson Gay, kutoka Marekani na Asafa Powell wa Jamaica -- wamepatikana na kosa kutumia madawa ya kusisimua misuli.

Gay, ambaye ni mwanariadha wa pili kwa kuwa na kasi kubwa ya kukimbia katika mbio za mita mia moja, amesema anajiondoa kwenye mashindano ya dunia ya riadha yanayotarajiwa kufanyika mjini Moscow mwezi ujao.

Asafa Powell, ambaye alishikilia rekodi ya mbio za mita 100 hadi ilipovunjwa na Usain Bolt mwaka 2008, amekanusha kuwa alitumia dawa hizo makusudi.

Mwanariadha mwenzake wa Jamaica Sherone Simpson pia amepatikana na hatia ya kuzitumia dawa hizo za kusisimua misuli.