Rais Bouteflika arejea nyumbani

Image caption Rais Abdelaziz Bouteflika

Rais wa Algeria, Abdelaziz Bouteflika amerejea nyumbani kutoka paris Ufaransa ambako amekuwa akipokea matibabu kwa muda wa miezi mitatu iliyopita.

Rais huyo mwenye umri wa miaka sabini na sita, alikumbwa na mshtuko wa moyo mwezi april na alisafirishwa hadi nchini ufaransa kwa matibabu.

Rais Bouteflika amekuwa madarakani tangu mwaka wa elfu moja mia kenda na tisini na tisa.

Wengi wanahisi kuwa hali yake ya afya huenda ikamzuia kuwania muhula mwingine kama rais katika uchaguzi mkuu unaopangiwa kufanyika mwaka ujao.