Shule za msingi zafungwa Kenya.

Wanafunzi shuleni Kenya
Image caption Wanafunzi shuleni Kenya

Serikali nchini Kenya imetangaza kufungwa kwa shule zote za msingi za umma kufuatia mgomo wa walimu ulioingia wiki ya nne sasa.

Waziri wa elimu Prof. Jacob Kaimenyi amesema kuwa shule hizo zitabakia kufungwa kwa muda usiojulikana.

Ameshutumu walimu akisema kuwa mgomo wao ulikuwa kinyume cha sheria.

Zaidi ya walimu 240,000 wamesusia kutoa mafunzo kwa wanafunzi wakidai nyongeza ya 500% ya mishahara waliyoahidiwa na serikali mwaka wa 2007.

Pia wanataka kuongezewa marupurupu ya usafiri, ya nyumba na matibabu. Serikali imesema kuwa wazazi wataarifiwa juu ya siku ya kufunguliwa tena shule.

Waziri huyo wa elimu Pro. Kaimenyo amesema kuwa wizara yake itafanya mipango maalum kwa ajili ya wanafunzi wa darasa la 8 wanaotarajiwa kufanya mtihani wao wa kitaifa chini ya miezi minne ijayo.