Israeli yawaachia wafungwa 100 Palestina

Image caption Mmoja wa wafungwa wa Palestina kwenye gereza Israeli

Baraza la mawaziri la Israeli limepitisha uamuzi wa kuwaachilia huru wafungwa zaidi ya mia moja wa Kipalestina kama sehemu ya juhudi za kuanzisha upya mazungumzo ya amani.

Kuachiliwa kwa wafungwa ambako kulipitishwa kwa kura thelathini dhidi ya tatu zilizopinga baada ya baraza kuketi,

Unatarajiwa kufanya kazi mapema iwezekanavyo miezi michache ijayo.

Vyanzo mbalimbali vinasema mazungumzo ya awali yanatarajia kufanyika mapema wiki hii mjini Washington.

Baraza hilo pia limepitisha muswada wa sheria wa makubaliano na Palestina ikiwemo la kuwekwa suala la kimipaka katika kura ya maoni.

Taarifa kutoka ofisi ya waziri Mkuu Benjamini Netanyahu imesema itakuwa ni muhimu kwa kila raia kupiga kura ya moja kwa moja katika maamuzi hayo ya kihistoria.