Wanyarwanda wapiganaji wa M23

Wapiganaji wa M23

Raia wanne wa Rwanda wameambia BBC kwamba walilazimishwa na jeshi la nchi hiyo kujiunga na waasi wa M23 Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Wanne hao wamesema walitoroka mapigano na kwamba wanajaribu kuomba hifadhi katika nchi jirani ya Uganda.

Mmoja wa Wanyarwanda hao wamesema asili mia 90 ya wapiganaji wa M23 ni wanajeshi wa Rwanda.

Mwenzake ambaye ni mwanafunzi wa utabibu amesema amewahudumia wapiganaji 300 waliojeruhiwa kwa risasi.

Serikali ya Rwanda imekanusha kuunga mkono waasi wa M23. Msemaji wa jeshi la Rwanda Joseph Nzabamwita amesema wanne hao wanatumia kisingizio cha kulazimishwa jeshini ili kupata hifadhi.