Ilani yatolewa kuhusu maziwa New Zealand

Serikali ya New Zealand imeonya kwamba maziwa pamoja na maziwa ya watoto wachanga kutoka kampuni moja maarufu, huenda yana bacteria wanaosababisha kupoooza, bacteria wa botulism.

Uchina tayari imetaka bidhaa hizo zirudishwe na kuagiza bidhaa zote zinazoingia nchini humo kutoka New Zealand zikaguliwe.

Kampuni kubwa ya maziwa ya Fonterra imesema imewaarifu wateja wake katika nchi kadhaa pamoja na Australia, Thailand, Malaysia, Vitenam na Saudi Arabia dhidi ya kutumia bidhaa hizo.

Inafikiriwa bacteria hao wanatoka kwenye mabomba ambayo hayakusafishwa sawa-sawa.

Gary Romano, ni mkuu wa kampuni ya Fonterra nchini New Zealand na amesema kampuni yake inajitahidi kudhibiti tatizo hilo:

"Tuna wasi-wasi sana sana juu ya afya ya binaadamu, na tunafanya kila tuwezalo kuzuwia bidhaa zisifikie wateja. Mimi nataka kuzungumza juu ya watu, siyo kampuni."