Rouhani aapishwa bungeni

Hassan Rouhani ameapishwa kuwa rais mpya wa Iran.

Bwana Rouhani aliahidi kuimarisha uchumi na kuleta haki na uhuru kwa Wairan wote kufuatana na katiba ya Iran.

Piya aliahidi kulinda mipaka ya nchi.

Sherehe hiyo ilifanywa bungeni mjini Tehran, ambako viongozi wa nchi kadha na wawakilishi wa mataifa ya nje walihudhuria.

Kuhusu mashauri ya nchi za nje, Hassan Rouhani alisema uhusiano na nchi nyengine utakuwa na msingi wa kuheshimiana na kupunguza uhasama.

Alisema Iran inataka amani na utulivu katika eneo zima, na haipendi serikali kubadilishwa kwa utumiaji nguvu.

Alisema uwazi, kuheshimiana na kupunguza vita ndio msingi wa kuanza ukurasa mpya katika uhusiano na nchi nyengine.