Wanajeshi zaidi wahitajika Somalia

Uganda imetoa wito wanajeshi zaidi wa Afrika wapelekwe katika kikosi kilioko Somalia, ili kikosi hicho kiweze kujizatiti katika maeneo iliyoyakomboa kutoka wapiganaji wa Kiislamu, Al Shabaab.

Waziri wa Mashauri ya Nchi za Nje wa Uganda, Sam Kutesa, alisema kati ya wanajeshi 2,000 hadi 20,000 zaidi wanafaa kupelekwa Somalia.

Viongozi wa nchi zilizochangia wanajeshi wanakutana na rais wa Somalia mjini Kampala, Uganda.

Msemaji wa rais wa Somalia, Abdirahman Omar Osman, alieleza kuwa kikosi cha kimataifa kitawekwa katika mji muhimu wa Kismayo.

Somalia imewashutumu wanajeshi wa Kenya walioko Kismayo kwamba wana msimamo wa upendeleo.