Wapigaji kura Mali wachagua rais

Wananchi wa Mali wanapiga kura katika duru ya pili ya uchaguzi wa rais - uchaguzi unaotarajiwa kurejesha demokrasi na utulivu baada ya matafaruku wa mwaka mzima chini humo.

Katika mwaka uliopita kumetokea vita na hatua za kijeshi zilizoongozwa na kikosi cha Ufaransa dhidi ya wapiganaji Waislamu na wa kabila la Tuareg kaskazini mwa nchi.

Makubaliano ya kusitisha mapigano, yaliyowezesha eneo la kaskazini kushiriki kwenye uchaguzi, piya yanaelekeza kuwa serikali mpya ianze mazungumzo na wale wanaotaka kujitenga katika muda wa miezi miwili.

Wapigaji kura wataamua juu ya wagombea wawili, aliyekuwa waziri mkuu Ibrahim Boubacar Keita ama Soumaila Cisse aliyewahi kuwa waziri wa fedha.