UN yawasili Syria - Kuna silaha za sumu?

Image caption UN kuchunguza utumiaji wa silaha za sumu Syria

Wachunguzi wa Umoja wa mataifa wamewasili nchini Syria kuchunguza madai kuwa pande zote mbili zinazopigana zimekuwa zikitumia silaha za sumu.

Waandishi wa habari walioko nje ya hoteli yao wanasema kuwa maafisa ishirini wameshawasili.

Hata hivyo hawakutoa taarifa yoyote. Awali Umoja huo ulitoa taarifa kuwa serikali ya Syria imekubali ujumbe wake ukiongozwa na mwansayansi kutoka Sweden Ake Sellstrom, kuja kufanya uchunguzi kwa kipindi cha wiki mbili.

Wanatarajiwa kuzuru maeneo matatu ikiwemo Aleppo ambapo serikali ya Syria imedai kuwa waasi walitumia silaha za sumu katika shambulio mwezi Machi.