Mahakama yaamuru Mubarak achiliwa

Image caption Hosni Mubarak

Mahakama mjini Cairo imetoa amri ya kuachiliwa huru kwa aliyekuwa rais wa Misri Honsi Mubarak.

Mahakama hiyo imeamuru Mubarak kuachiliwa huru kutokana na mashitaka ya rushwa yaliyokuwa yanamkabili.

Lakini bado haijajulikana kama ataachiliwa baadaye jumatano ya leo.

Upande wa mashitaka unatarajiwa kukata rufaa.

Kiongozi huyo wa zamani mwenye umri wa miaka 85 anakabiliwa pia na kesi ya kushiriki kwenye mauwaji ya malefu ya raia walioandamana kwenye vuguvugu la mapinduzi lililomtoa madarakani mwaka 2011.

Alifungwa kifungo cha maisha jela mwaka jana, lakini alikata rufaa na kushinda na kesi yake kutakiwa kusikilizwa upya.