Kesi dhidi ya Bo Xilai imekamilika

Image caption Bo Xilai

Upande wa mashtaka katika kesi ya mwanasiasa mashuhuri nchini Uchina Bo Xilai, umetoa taarifa yake ya mwisho dhidi ya kiongozi huyo ambaye awali alitarajiwa na wengi kuchukua uongozi wa taifa hilo.

Katika taarifa hiyo, waendesha mashtaka wamesema kuwa kiongozi huyo wa zamani hafai kupewa hukumu hafifu kutokana na uzito wa mashtaka yanayomkabili ya ufisadi na utumizi mbaya wa mamlaka.

Bo Xilai sasa ana fursa ya kuzungumzia kuhusu shinikizo za kisiasa mbali na kuwakosoa wapinzani wake.

Mwandishi wa BBC anasema kwamba licha ya kuwa kulikuwa na uwazi wakati wa kusikilizwa kwa keshi hiyo, kesi hiyo bado inadhibitiwa na chama cha Kikomunisti.