Watu 40 wauawa Iraq

Image caption Shambulio la Bomu Baghdad

Takriban watu 40 wameuawa nchini Iraq na wengine zaidi ya mia moja wakijeruhiwa katika misururu ya mabomu yaliotegwa katika mji mkuu wa nchi hiyo Baghdad.

Polisi wanasema kuwa milipuko hiyo ilitokea katika maeneo yanayokaliwa na watu wa dhehebu la shia.

Shambulio baya zaidi lilitokea katika eneo la Jisr al-Diyala Kusini Mashariki mwa mji huo.

Polisi wanasema kuwa mabomu mawili yalilipuka Kazkazini mwa wilaya ya Kazimiyah.

Haya ni mashambulio mapya kufanyika katika mji wa Baghdad mwezi huu.

Waandishi wanasema kuwa mashambulizi yanayotekelezwa na watu wa dhehebu la suni dhidi ya wale wa dhehebu la shia yameongezeka mwaka huu.