Kesi ya daktari wa Bin Laden kusikiliwa upya

Image caption Shakil Afridi

Maafisa wa serikali ya Pakistan, wamefutilia mbali hukumu ya kifungo gerezani aliyopewa daktari aliyewasaidia maafisa wa ujasusi wa Marekani CIA kumsaka Osama Bin Laden.

Ripoti zinasema serikali imegaiza kesi hiyo dhidi ya Shakil Afridi kusikilizwa upya.

Shakil Afridi, alishtakiwa na kosa ya uhaini na kufunguliwa mashtaka chini ya sheria za kiukoo kwa kuendesha shughuli bandia ya kutoa chanjo kwa watoto ili kukusanya habari.

Daktari huyo alihukumiwa kifungo cha miaka thelathini gerezani mwaka wa 2012, na tangu wakati huo amekuwa akizuliwa katika gereza moja mjini Peshawar.

Bin Laden, aliuawa na wanajeshi wa Marekani mwezi Mei mwaka wa 2011 katika eneo la Abbottabad nchini Pakistan.

Kuuawa kwa Bin Laden, kulisababisha mzozo mkali wa kidiplomasia kati ya Marekani na Pakistan ambayo ilidai operesheni hiyo ilikiuka uhuru wake.